Ziara ya rais uhuru kenyatta nchini uchina ilikuwa na manufaa makubwa kwa wafanyibiashara nchini.
Kulingana na msemaji wa ikulu BI Kanze Dena ziara hiyo iliyokuwa na ujumbe wa zaidi ya wafanyi biashara 100 wa matunda kutoka hapa nchini ilifanikisha kutiwa saini kwa mkataba wa makubaliano baina ya kenya na uchina ilikufanikisha wafanyibiashara kupata soko la kuuza bidhaa zao .
Akizungumza na wanahabari katika ikulu ya rais mjini mombasa bi Kadze amefichua kuwa ziara hiyo ilisaidia pakubwa kupigajeki wafanyibiashara wa kenya kuuza bidhaazao katika taifa la uchina.
Bi Kanze aidha amefichua kuwa ziara hiyo itasaidia pakuwa sekta ya biashara kuinuka kwa kiasi kikubwa na kuinua uchumi wa taifa.
Itakumbukwa kuwa siku chache ziliozopita rais Uhuru Kenyatta aliongoza ujumbe wa zaidi wa wafanyibiashara 100 nchini China ambapo alitia saini mkataba wa makubaliano na uchina kuwa na soko huru la uuzaji wa bidhaa mbalimbali nchini humo.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.