Picha kwa hisani –
Rais Uhuru Kenyatta amepongeza shirika la Maendeleo ya Wanawake kwa kuwa katika msitari wa mbele kupigania haki za wanawake nchini.
Akizungumza wakati wa mkutano wa kila mwaka wa shirika hilo Kenyatta amesema shirika hilo limeongoza juhudi ambazo zimebadilisha na kuboresha maisha ya wanawake hasa katika sehemu za mashambani.
Kiongozi wa nchi amesema mafunzo yanayotolewa na shirika hilo la maendeleo ya wanawake kuhusu ukulima ili kuimarisha kujitosheleza kwa chakula katika ngazi za familia,yanayosaidia kupiga jeki agenda ya serikali ya usalama wa chakula.
Kwa upande wake waziri wa utumishi wa umma na Jinsia Prof Margaret Kobia amesema shirika hilo linashiriki katika ustawi wa kitaifa kwa kutoa mwongozo bora wa kuimarisha kiwango cha maisha ya familia na jamii.
Naye mwenyekiti wa shirika hilo Rahab Muiu amesema wanaunga mkono marekebisho yanayoendelea ya kikatiba akisema kwamba mchakato wa BBI utaleta mwamko mpya wa umoja wa kitaifa, amani na maendeleo.