Picha kwa Hisani –
Rais Uhuru Kenyatta ametoa agizo la kubuniwa kwa mfumo wa usimamizi, ushirikishi na Muungano wa huduma za umma zinazohusiana na bandari, reli na mabomba ya mafuta ya petroli nchini KTLN.
Kiongozi wa nchi, amesema mfumo huu mpya unatarajiwa kusaidia kupunguza gharama ya kufanya biashara nchini kupitia utoaji wa muundo msingi wa bandari, reli na mabomba ya mafuta kwa gharama nafuu.
Rais Kenyatta, amesema mashirika hayo manne ya serikali yatakuwa chini ya Hazina ya Kitaifa kwa mjibu wa mapendekezo ya jopokazi la Rais kuhusu marekebisho ya mashirika ya serikali.
Katika utaratibu huo mpya, Shirika la ustawi wa viwanda na Biashara (ICDC) litakuwa mmiliki wa mashirika hayo matatu na kusimamia uekezaji wa serikali katika huduma za bandari, reli na mabomba ya mafuta ya petroli.