Picha kwa hisani –
Rais Uhuru Kenyatta amefanya mabadiliko ya uongozi katika taasisi mbali mbali za serikali nchini,ambapo Lewis Nguyi ameteuliwa kama mwenyekiti wa bodi ya hazina ya NHIF na kuchukua nafasi ya Hannah Muriithi alieshikilia wadhfa huo tangu mwaka 2018.
Kwenye mabadiliko hayo yaliyoyachapishwa katika gazeti rasmi la serikali Rais Kenyatta amemteua Sitoyo Lopokoiyot kama mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya mafunzo ya ‘Moi teaching and referral hospital’ MTRH.
Lopokoiyot amechukua nafasi ya aliyekua mbunge wa Eldoret Joseph Lagat na ataanza rasmi kuhudumu tarehe 29 ya mwezi ujao wa Machi.
Rais Kenyatta vile vile amemteua Dkt Daniel Mbinda Musyoka kama mwenyekiti wa bodi ya taasisis ya utafiti wa matibabu nchini KEMRI na kufutilia mbali uteuzi wa Naftali Agata.