Picha kwa hisani –
Rais uhuru Kenyatta ameongoza uzinduzi wa kituo cha mizigo cha reli katika makao makuu ya shirika la reli yaliyoko jijini Nairobi mapema leo.
Kituo hicho kitakachojulikana kama BomaLine, kinalenga kuwasaidia wafanyibiashara wadogo nchini kuwawezesha kuingiza na kutoa mizigo jijini Nairobi.
Katika uzinduzi huo Rais Kenyatta ametaja kituo hicho kwamba kitapunguza msongamano wa wafanyibiashara bandarini na pia kupunguza utapeli unaofanyiwa wanabiashara.
Uhuru vile vile amewasihi wale walioko serikalini kuwasaidia wafanyibiashara wadogowadogo katika ufanyikazi wao bali sio kuwaongezea shida.