Picha kwa hisani –
Rais wa Marekani Donald Trump amemshinikiza Gavana wa jimbo la Georgia wa chama cha Republican kumsaidia kupindua ushindi wa Joe Biden jimboni humo.
Katika mfululizo wa ujumbe alizotuma kupitia mtandao wa Twitter, Trump amemtaka mgombea Brian Kemp kuitisha kikao maalum cha bunge.
Hatua hiyo inawadia saa kadhaa baada ya Trump kuhudhuria mkutano wa kampeni huko Georgia wakati jimbo hilo linajitayarisha katika marudio ya uchaguzi wa Seneti.
Hata hivyo Rais Trump bado amekataa kukubali kuwa alishindwa katika uchaguzi mkuu, akidai kuwa ulikuwa na wizi wa kura ingawa hajawahi kutoa ushahidi wowote kuthibitisha kuwa ushindi wa Joe Biden ulitokana na wizi wa kura.
Trump amefungua kesi Mahakamani katika majimbo kadhaa lakini hadi kufikia sasa kesi zote zimeshindwa kufaulu.