Story by Our Correspondents-
Rais William Ruto amewahakikisha watahiniwa wa mitihani ya kitaifa nchini KCPE na ule wa KPSEA kwamba usalama wao umeimarishwa na hawafai kuhofia lolote bali kufanya bidii katika mitihani hiyo.
Akizungumza baada ya kushuhudia ufunguzi wa kasha la mtihani wa somo la Sayansi katika shule ya msingi ya Joseth Kang’ethe jijini Nairobi, Rais Ruto amesema serikali itahakikisha hakuna visa vya udanganyifu vinashuhudiwa.
Rais amewaagiza wasimamizi wa mitihani hiyo ya kitaifa kushirikiana na maafisa wa usalama kuhakikisha mitihani hiyo inafanyika bila ya changamoto zozote.
Wakati uo huo amewataka viongozi wengine wa serikali kuhakikisha swala la elimu inazingatiwa kikamilifu nchini ili kufanikisha ndoto za wanafunzi wengi.