Story by Our Correspondents–
Rais William Samoei Ruto amemteua Amin Mohammed Ibrahim kuwa Mkurugenzi mkuu wa idara ya upelelezi wa jinai nchini DCI.
Katika tangazo lililochapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali, Rais Ruto amemteua Ibrahim kushikilia nafasi hiyo iliyoachwa wazi na George Kinoti baada ya kujiuzulu.
Ibrahim anatarajiwa kuanza majukumu yake rasmi baada kuapishwa kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo Ibrahim atakuwa na kibarua kigumu cha kutegua kitendawili cha sakata za ufisadi ambazo zimekuwa changamoto kukabiliwa wakati nafasi hiyo ilipokuwa ikishikiliwa na Kinoti.
Sintofahumu za watu kupotea katika hali tatanishi ni maswala ambayo wakenya wengi hasa kutoka eneo la Pwani wanatarajia kuona yakikomeshwa na usalama kuimarishwa.