Story by: Mwahoka Mtsumi
Rais William Ruto amefungua rasmi Kongamano la viongozi wa mashtaka ya umma linalolenga kuboresha utendakazi bora na ushirikiano wa Afrika ili kufanikisha usawa na haki Mahakamani.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo la 16 linalojumuisha mataifa 43, Rais Ruto amesema viongozi wa mashtaka wa jukumu la kuhakikisha bara la afrika linapiga hatua katika ufanikishaji wa katiba, siasa na uongozi bora.
Kiongozi wa taifa amesema mikakati bora iliyowekwa utawezesha viongozi hao kukabiliana na ufisadi, dhulma za jinsia, ugaidi maswala mengine tata barani afrika ili kuhakikisha mfumo wa haki za jinai unaangaziwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa mshataka ya umma humu nchini Noordin Hajj ameweka wazi kwamba kupitia mikataba bora iliyowekwa itachangia bara za afrika kuzingatia muongozo wa Katiba na sheria katika kushughulikia kesi Mahakamani.
Naye mkurugenzi wa mashtaka ya umma kutoka taifa la Nigeria Babadogo Mohamed amesema ugaidi na itikadi kali ni changamoto katika bara la afrika na kushinikiza idara husika sawa na viongozi wa mashtaka kushirikiana kimawazo na kulikabili tatizo hilo.
Wakati uo huo Mkurugenzi wa mashtaka ya umma kutoka taifa la Afrika Kusini Wakili Shamila Patoi amewahimiza viongozi wa mashtaka ya umma kuzingatia sheria katika utekandazi wao sawa na kujitenga na ushawishi wa kisiasa.