Picha kwa hisani –
Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga wameipokea rasmi ripoti ya BBI katika ikulu ndogo ya Kisii.
Akizungumza baada ya kupokea ripoti hio asubui ya leo rais Kenyatta amewasihi wakenya kutenga muda wao na kuisoma kikamilifu ripoti hio kabla ya kufanya maamuzi.
Kenyatta amesema wakenya na kuibuka na mtazamo huru usiyo na muingilio wa mtazamo wa kisiasa kuhusu ripoti hio bora kabla ya kuinga mkono au kuipinga ripoti hio.
Rais Kenyatta vile vile amelitaka jopo la maridhiano kuhakikisha ripoti hio ambayo inalenga kulinda haki za wakenya inasambazwa kwa wakenya wote kabla ya siku ya jumatatu jumalijalo ili wapate fursa ya kuisoma.
Kwa upande wake kinara wa ODM Raila Odinga amesema ripoti hio itamaliza matatizo yanayowakabili wakenya wa kaunti mbali mbali ikiwemo dhulma za kihistoria za ardhi ,umaskini miongoni mwa matatizo mengine.
Ripoti hio itazinduliwa rasmi kwa umma siku ya jumatatu jumalijalo katika ukumbi wa BOMAS jijini Nairobi.