Picha kwa hisani –
Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga wameanza kampeni ya kuupigia debe mchakato wa kuwaunganisha wakenya wa BBI katika kaunti ya Kisumu.
Rais Kenyatta amewahimiza wakenya kuiunga mkono ripoti ya BBI aliyokabidhiwa rasmi na Jopokazi la maridhiano nchini BBI chini ya Mwenyekti wake Yusuf Hajj.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kiserikali katika kaunti ya Kisumu, Kiongozi wa nchi amewahimiza wakenya kuisoma kwa kina ripoti hiyo pindi itakapowasilisha mashinani kabla ya kufanya maamuzi ya kuiunga mkono au la.
Rais Kenyetta, hata hivyo amesema Handshake imeleta mabadiliko makubwa nchini kwani sasa taifa limeshuhudia amani na maendeleo huku akiwaahidi wakenya kuwa hakuna machafuko yatakayoshuhudiwa tena humu nchini.
Kwa upande wake Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga aliyeandamana na Rais Kenyatta katika kaunti hiyo, amesema BBI itasitisha ufisadi nchini pamoja na kuchangia uchaguzi huru na amani.