Picha Kwa Hisani –
Rais Uhuru Kenyatta hii leo amevunja kimya chake na kuzungumzia sintofahamu iliyopo wa mvutano wa ugavi wa raslimali kwa serikali za kaunti.
Akizungumza wakati wa halfa ya ugavi wa hati miliki za ardhi elfu 38 kwa wakaazi wa Nairobi katika jumba la mikutano la KICC, Rais Kenyatta amesema hajahusika kivyovyote na mvutano huo mfumo wa ugavi wa mapato ulioamuliwa na Tume ya ugavi wa raslimali nchini CRA.
Kiongozi wa nchi, amesema swala muhimu kwa sasa ni kuwahudumia wakenya na wala sio kujihusisha na maswala yasiofaa kwani wananchi wanahitaji hudumu mbalimbali mashinani.
Kwa upande wake Naibu Rais Dkt William Ruto, amesema japo ni vyema kwa kaunti zilizo na idadi kubwa ya watu kupokea mgao mkubwa wa raslimali, ni vyema pia kaunti zilizo na idadi ndogo ya watu kufikiriwa kwa undani.