Story by Our Correspondents –
Viongozi wa chama cha Jubilee wamempendekeza Rais Uhuru Kenyatta kuendelea kushikilia nafasi ya Kinara wa Chama hicho hata baada ya kustaafu kama Rais mwezi Agosti mwaka huu.
Katika mkutano wa wajumbe wa chama hicho ulioandaliwa katika Ikulu ya Nairobi, wajumbe hao wamesema Rais ataendelea kuongeza chama hicho ili kuwepo na muungano dhabiti ya kisiasa.
Wajumbe wa chama hicho wakiongozwa na Katibu mkuu wao Raphael Tuju wamekubaliana kutoidhinisha mgombea yoyote wa Rais wakati wa uchaguzi mkuu ujao na badala yake kushirikiana na vyema vingine ili kuunda serikali ijayo.
Hata hivyo viongozi hao wamepinga madai yaliokuwa yakienezwa kwamba chama hicho hakina wafuasi tena, wakidai kwamba bado chama cha Jubile kiko imara.