Picha kwa hisani –
Rais Uhuru Kenyatta ameyakosoa vikali mataifa ya kigeni yanaolenga kuvuruga maswala ya ndani ya Kenya, akisema serikali ya Kenya haitakubali mataifa hayo kuvuruga amani nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jumba la G47 ambalo litakuwa makao ya serikali za ugatuzi sawia na mikakati ya kufufua uchumi wa taifa, Rais Kenyatta amesema japo Kenya inashukuru mchango wa unaotolewa mataifa ya Ulaya, ni vyema mataifa hayo kuheshimu taifa la Kenya.
Kiongozi wa nchi, ameyataka mataifa hayo kukoma kuingilia undani wa mipango ya Kenya pamoja na kushauri jinsi wakenya wanavyofaa kufanya, akisema wakenya wana uwezo wa kujisimamia wenyewe.
Wakati uo huo amezitaka serikali za kaunti kutumia vyema fedha zilizotengewa sekta mbalimbali nchini ikiwemo zile za kuboresha uchumi wa nchi ili kuhakikisha maazimio ya serikali ya kuwahudumia wananchi yanatimia.