Picha kwa hisani –
Rais Uhuru Kenyatta amewaomba wakenya waunge mkono mchakato wa kuifanyia marekebisho Katiba wa BBI, akisema wananchi watanufaika na mengi yaliomo ndani ya BBI ikiwemo rasilimali zitasambazwa kwa wingi mashinani.
Rais Kenyatta amewataka pia wakenya wajihadhari na wanasiasa wanaopinga mchakato wa BBI, akisema hawana ukweli wowote katika pingamizi zao kuhusu BBI.
Kiongozi wa taifa yamekuwa yakiyazungumza yao katika Ikulu ndogo ya Sagana ambako alihutubia zaidi ya viongozi 7,000 kutoka eneo la Mlima Kenya na kaunti jirani wakati wa siku yake ya pili ya ziara ya kikazi katika eneo hilo.
Rais amesema alishauriana kwa kina na kuafikiana na wadau mbali mbali kabla ya kuzindua mchakato wa BBI, ambao nia yake ni kulinda haki na uhuru wa kila mmoja.
Katika mkutano huo Rais Kenyatta amekiri kujitolea kwake kuacha urathi wa nchi yenye amani na umoja ambapo kila Mkenya atafurahia haki yake ya kijamii, kiuchumi na kisiasa bila ya hofu ya kuingiliwa, akisema BBI itasaidia kuafikia lengo hilo.