Picha kwa hisani –
Rais Uhuru Kenyatta amesema ameridhishwa na mikakati ilioidhinishwa na wadau wa sekta ya utalii nchini ya kuwakinga watalii dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.
Akizungumza katika Ikulu ya Nairobi kupitia njia ya kidijitali, rais Kenyatta amesema Kenya iko tayari kupokea watalii, akiwahimiza watalii wa kigeni na wakinyumbani kutumia fursa ya punguzo la bei katika vivutio vya watalii na kutembelea maeneo hayo.
Kiongozi wa nchi, amewataka wakenya pamoja na wageni wanaozuru taifa hili kuendelea kuyazingatia maagizo ya kuepuka maambukizi ya virusi vya Corona, akiseme kila mmoja anajukumu la kujilinda.
Kwa upande wake Waziri wa Utalii nchini Najib Balala aliyezungumza katika mkao huo ameishukuru serikali kwa kutenga fedha za kufufua sekta ya utalii, akisema fedha hizo zitatumika katika kuboresha mbuga za wanyamapori.