Story by Our Correspondents –
Rais Uhuru Kenyatta amewahimiza wakenya na wanasiasa nchini kuhakikisha wanafanya siasa za amani , akisema hatua hiyo ndio itakayochangia taifa hili kushuhudia amani.
Akizungumza baada ya kuhudhuria ibada ya Jumapili katika Kanisa la AIC Pipeline jijini Nairobi, Rais Kenyatta amewakosa wale wenye mazoea ya kuwashambulia wanasiasa wengine katika majukwaa ya kisiasa, akihoji kwamba tabia hiyo haifai.
Kiongozi wa taifa amewasisitiza wanasiasa na wafuasi wao kutambua umuhimu wa amani na uzalendo, akiwataka wanasiasa kukubali matokeo ya uchaguzi.
Akigusia swala la uhaba wa mafuta na kupanda wa bei ya mafuta nchini, Rais Kenyatta amesema japo swala hilo limechangiwa na vita vinavyoendelea nchini Ukraine swala hilo litapata suluhu hivi karibuni kwani mazungumzo ya kusitisha vita hivyo yanaendelea.
Wakati uo huo amesema wakati umefika sasa kwa wakenya kuungana na kuendeleza demokrasia ya nchi kwa kuhakikisha wakenya wanajitenda na siasa za vurugu.