Story by Our Correspondents –
Rais Uhuru Kenyatta amewataka wananchi na wanasiasa kote nchini kuzingatia swala la amani, uwiano na utangamano wa kijamii katika mikutano yao ya kisiasa na kuuza sera zao vyema ili kuhakikisha taifa hili linajitenga na siasa za vurugu.
Kiongozi wa taifa amesema hakuna taifa linaloweza kuendelea kimaendeleo iwapo litasheheni siasa za vurugu, akisisitiza umuhimu wa kila mmoja kuzingatia amani na mshikamano wa taifa.
Akizungumza wakati wa halfa ya mazishi ya Mama Loise Njeri Mbugua katika kijiji cha Karinde kaunti ya Kiambu, Rais Kenyatta amesema japo demokrasia ni haki ya kila mmoja haifai kutumika vibaya na kuwakandamiza wengine.
Wakati uo huo amewashauri wakenya kufanya maamuzi ya busara wakati wa kuwachagua viongozi wanaolenga kuwatumikia katika kipindi cha miaka mitano ijayo ili taifa hili lishuhudie maendeleo.