Picha kwa Hisani –
Rais Uhuru Kenyatta ameiagiza Wizara ya Afya nchini kuchapisha habari zote za ununuzi wa vifaa vinazohusiana na maradhi ya Covid-19 hasa vilivyonunuliwa na Shirika la usambazaji dawa nchini, KEMSA.
Rais Kenyatta, amesema kuchapishwa kwa habari za ununuzi wa vifaa ikiwemo washindi wa zabuni ni hatua ya uwazi ya kukabiliana na ufisadi ambayo inafaa kuigwa na mashirika yote ya umma.
Kiongozi nchi, ameyasema hayo katika Ikulu ya Nairobi wakati wa kikao cha kufunga kongamano la Covid-19 kwa njia ya video lililoandaliwa na Baraza la Magavana nchini kuhusu kubuni mikakati ya kukabiliana na Covid-19 kwa serikali za kaunti.
Wakati uo huo ameiagiza Wizara ya Afya nchini kuipa kipaumbele huduma za afya ya akili, akisema hali hiyo imekuwa changamoto kubwa Wakenya wengi, hasa vijana.