Story by Our Correspondents –
Serikali ya Kenya imewahakikishia wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali kwamba Kenya iko salama kwa biashara na wawekezaji wako na nafasi ya kuendeleza biashara zao humu nchini.
Kauli hiyo imetokewa na Rais Uhuru Kenyatta wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya kitaifa ya maonyesho katika nchi za miliki za kiarabu mjini Dubai ambapo Rais amesema utawala wake umeweka mikakati mwafaka kwa uwekezaji.
Rais Kenyatta amesema sheria zilizobuniwa nchini zinawalinda wawekezaji wa viwango vya kimataifa ikiwemo ulinzi wa mali zao huku akisema Kenya imekubali mipango inayoendelezwa na mataifa ya miliki za kiarabu katika swala la uwekezaji.
Hata hivyo maonyesho hayo inatarajiwa kuendelea kwa kipindi cha mwezi mmoja huku mataifa mbalimbali yakipangiwa kuonyesha bidhaa zao sawa na kuwavutia wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali.