Picha kwa hisani –
Rais Uhuru Kenyatta ametia saini kuwa sheria mswada wa marekebisho ya Tume ya IEBC ya mwaka 2019 na mswada wa matangazo kwa serikali za kaunti wa mwaka 2020.
Katika sheria hiyo, sasa Tume ya IEBC itatoa fursa ya kuchaguliwa kwa jopo maalum litakalosimamia shughuli ya kuteuliwa kwa makamisha wa kuziba nafasi zilizowazi katika tume hiyo.
Sheria hiyo vile vile imetoa muongozo wa kuchaguliwa kwa makamishna wa IEBC na itatoa vigezo kamili kwa wanaostahili kuchaguliwa kama jopo la uteuzi katika tume hiyo.
Katika sheria ya matangazo kwa serikali za kaunti, sheria hiyo inatoa muongozi wa matangazo kuhakikisha kuna kuwa na usawa katika sekta ya biashara, mazingira na afya ya umma na inalenga kuongeza ushuru kwa kaunti zote 47 nchini.