Rais Uhuru Kenyatta amewataka wabunge kuipa kipaumbele miswada inayolenga kupiga kufanikisha ajenda nne kuu za serikali.
Akizungumza katika kikao na wakuu wa bunge la kitaifa na Seneti katika Ikulu ya Nairobi, Rais Kenyatta amesema kuna miswada mingi muhimu ambayo haijajadiliwa kufuatia mivutano inayoshuhudiwa miongoni mwa viongozi katika mabunge hayo.
Kwa upande wake Spika wa bunge la Seneti Ken Lusaka amempongeza Kiongozi wa nchi kwa kuingilia kati sintofahamu kuhusu ugavi wa mapato na kumhakikishia kujitihadi kwa Bunge la Seneti kuunga mkono ajenda ya serikali.
Naye Spika wa bunge la kitaifa Justine Muturi amependekeza kubuniwa kwa afisi ya ushirikiano katika kila Wizara ili kufanikisha ajenda za serikali.
Hata hivyo Kiongozi wa wengi katika Bunge la Seneti Samuel Poghisio na Kiongozi wa wachache katika bunge hilo James Orengo na wenzao katika bunge la taifa Amos Kimunya na John Mbadi pia walizungumza kwenye mkutano huo.