Story by Our Correspondents –
Rais Uhuru Kenyatta amesema kukamilika kwa kituo kipya cha kuhifadhi mafuta cha Kipivu katika kaunti ya Mombasa kutasaidia pakubwa kudhibiti bei ya mafuta nchini.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kufanya ziara ya ukaguzi katika kituo hicho cha mafuta cha Kipevu, Rais Kenyatta amesema kituo hicho ambacho kitapokea mafuta kutoka kwa Meli za kusafirisha mafuta kutoka mataifa mbalimbali ulimwenguni kitaimarisha uchumi wa nchi.
Kiongozi wa taifa amedokeza kwamba kituo hicho kitasaidia kuokoa hadi shilingi bilioni mbili kila mwaka ambazo zimekuwa zikitumika kulipa fidia kutokana na kucheleweshwa kwa mafuta.
Kwa upande wake Waziri wa Fedha nchini Ukur Yatan aliyeandamana na Rais Kenyatta katika ziara hiyo ya ukaguzi wa kituo cha mafuta cha Kipevu, amesema kituo hicho kimekamilika kwa asilimia 96 na kitaanza kutoa huduma mara moja.