Story by Our Correspondents –
Rais Uhuru Kenyatta amewapongeza wanajeshi wa Kenya kwa kujitolea kwao kulinda taifa hili katika kila pembe ya nchi ikiwemo ardhini, majini na Angani.
Rais Kenyatta amesema serikali imeboresha maslahi ya vikosi vya maafisa wa usalama nchini na kuviwezesha kuiweka Kenya katika ulinzi wa hali ya juu kwenye ramani ya kitaifa na kimataifa.
Akizungumza katika halfa ya kufuzu kwa makurutu wa jeshi la Cadet zaidi ya 168 wa ardhini, majini na angani katika kambi ya mafunzo ya kijeshi mjini Nakuru, Kiongozi wa taifa amesema chuo cha mafunzo ya kijeshi kimepewa cheti rasmi cha kuhudumu na kutoa ushauri nasaha.
Wakati uo huo amesisitiza mshikamano wa taifa kwa wakenya wote sawa na kuvipongeza vikosi vya usalama nchini kutokana na juhudi zao za kulinda taifa hilo.