Picha kwa hisani –
Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza haja ya kufanyiwa mabadiliko ya katiba ya nchini ili kuwezesha taifa kuandaa uchaguzi utakaojumuisha wananchi wa tabaka mbali mbali kwenye uongozi wa taifa.
Akizungumza wakati wa hafla ya mashujaa katika uwanja wa Gusii kaunti ya Kisii,Kenyatta amesema mabadiliko ya katiba yanalenga kuzidisha mshikamano wa wakenya na wala sio kubuni nafasi zaidi za uongozi kama inavyodaiwa.
Kenyatta vile vile amesema wadau mbali mbali wanapaswa kufanya majadiliano ya kina kabla katiba ya nchi kubadilishwa,ili kuhakikisha vipengele muhimu vitakavyozidisha umoja wa taifa vinajumuishwa.
Kwa upande wake naibu wa rais William Ruto ameipiga jeki kauli ya rais Kenyatta,akipendekeza kufanywa mazungumzo kabla mabadiliko ya katiba ya nchini kubadilishwa kupitia ripoti inayopigiwa upato ya BBI.
Naye kinara wa chama cha ODM Raila Odinga amesema hakuna atakayezuia mchakato wa BBI kwani ripoti hio inalenga kuwakomboa wakenya kwa kubadilisha vipengele kandamizi katika katiba ya sasa.
Siku ya mashujaa awali ilitambulika kama Kenyatta day na sherehe za leo ni za kumi na moja tangu sherehe hizo kupewa jina hilo la mashujaa day.