Picha kwa hisani –
Rais Uhuru Kenyatta ameongoza sherehe ya kufuzu kwa maafisa wa jeshi wa vyeo vya Cadet.
Akihutubu wakati wa hafla hio katika chuo cha mafunzo ya kijeshi cha Lanet kaunti ya Nakuru,Kenyatta amesema wakati huu ambapo kunaibuka changamato za kiusalama ulimwenguni ni lazima mafunzo ya wanajeshi yaangazie vitisho vya usalama vinavyoibuka.
Kenyatta amesema ili wanajeshi wa taifa wafanikiwe kuzikabili changamoto za kiusalama zinazoibuka kwa ujuzi wa hali ya juu na kwa ujasiri,ni lazima wanajeshi wazidi kuendeleza masomo yanayofungamana na kazi hio.
Maafisa hao wa Cadet wanaofuzu hii leo ni kundi la 8 lililosomea Shahada ya Sayansi katika maswala ya Kijeshi na Usalama kwenye mpango ulioandaliwa na Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Hafla hio imehudhuriwa na waziri wa ulinzi Balozi Monica Juma, mkuu wa majeshi Jemedari Robert Kibochi,wakuu wa vikosi na maafisa wengine wakuu serikalini.