Story by Rasi Mangale –
Rais Uhuru Kenyatta amezindua rasmi mashindano ya mbio za dunia za magari ya safari Rally (WRC) katika haklfa iliyofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano KICC, jijini Nairobi.
Ni miaka 19 tangu mbio hizo kufanyika nchini na sasa zinarudi tena na zitakuwa na wafanyikazi 58.
Dereva wa kwanza kuondoka alikuwa kutoka kabraza Sugar Racing Onkar Rai akiongozwa njia na Drew Sturrock, akifuatwa na Bingwa wa mbio za Equator African Rally Carl Tundo ambaye anaongozwa na Tim Jessop.
Rais Kenyatta ambAye ni kiongozi wa mbio za safari rally aliandamana na Rais wa FIA Jean Todt, Waziri wa michezo nchini Bi Amina Mohamed na mkurungezi mkuu mtendaji wa WRC Safari Rally Phineas Kimathi katika halfa hiyo.
Mbio hizo zitaanza rasmi siku ya Ijumaa hadi Jumapili.