Picha kwa hisani –
Rais Uhuru Kenyatta amezindua Idara ya kitaifa ya kushughlikia huduma za angani, ambayo ni kitengo kinachohusisha mashirika mbalimbali katika Wizara ya Ulinzi.
Akizunguumza katika makao makuu ya idara hiyo katika Uwanja wa ndege wa Wilson, Rais Kenyatta amesema idara hiyo ambayo inajumuisha raslimali zote za angani za serikali itaimarisha utendakazi bora wa safari za ndege.
Kiongozi wa nchi amesema mpango huu wa mabadiliko ulishurutishwa na haja kubwa ya kuimarisha utendakazi bora katika usimamizi wa mali ya kitaifa ya usafiri wa ndege kwa lengo la kuboresha usalama, utendakazi bora na kuboresha uwezo wa kupata ndege.
Hata hivyo Waziri wa Ulinzi nchini Dkt Monica Juma na mkuu wa majeshi nchini Robert Kibochi walizungumza kwenye hafla hiyo iliyohudhuriwa na maafisa wakuu serikalini akiwemo mkuu wa utumishi wa umma Joseph Kinyua.