Story by Correspondent –
Rais Uhuru Kenyatta amewateua Francis Wanderi, Justus Abonyo, Juliana Cherera na Irene Cherop kuwa Makamishna wa Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.
Rais Kenyatta amechukua hatua hiyo baada ya jopo la makamishna waliotikwa jukumu la kuwapiga msasa watu zaidi ya 30 waliokuwa wakitafuta nafasi hizo kukamilika.
Majina ya watu hao wanne yamewasilishwa katika bunge la kitaifa kupigwa msasa na iwapo bunge litaridhia uteuzi hao basi moja kwa moja wanne hao wataapishwa.
Watu hao wanne iwapo wataapishwa basi wataongeza idadi ya makamishna wa Tume ya IEBC nchini kuwa makamishna 7 kabla ya uchaguzi kuu kuandaliwa Augosti 9 mwaka wa 2022.