Story by Our Correspondents
Rais Uhuru Kenyatta ameteua jopo maalum la watu 7 ili kuchunguza madai ya ufisadi yanayomkabili Jaji wa Mahakama mkuu aliyesimamishwa kazi Said Juma Chitembwe.
Jopo hilo ambalo litaongozwa na Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mumbi Nguji, linajumisha Jaji Abida Ali Aroni, Jaji Nzioki wa Makau, Wakili Fred Odhiambo, James Ochieng Oduor, Jenerali mstaafu Jackson Ndungu na Lydia Nzomo.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Rais Kenyatta amesema madai yaliyoibuliwa dhidi ya Jaji Chitembwe yana uzito na huenda yakachangia wakenya kutokuwa na imani na idara ya Mahakama.
Hatua hiyo imejiri baada ya Rais Kenyatta mnamo tarehe 5 mwezi huu kupokea mapendekezo ya Tume ya huduma za mahakama nchini JSC kwa Jaji Chitembwe anafaa kuachishwa kazi.