Story by Our Correspondents –
Rais Uhuru Kenyatta ametangaza rasmi kuongelewa mara moja kwa kafyu kote nchini ili kuhakikisha taifa linaimarika kiuchumi baada ya kukabiliwa na changamoto za janga la Corona.
Rais Kenyatta amesema amechukua hatua hiyo baada ya kushuhudiwa kushuka kwa idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini sawia na wakenya kuzingatia kikamilifu kununi za kujikinga na virusi vya Corona.
Akihutubia wakenya wakati wa sherehe za mashujaa katika uwanja wa Wang’uru kaunti ya Kirinyaga, Rais Kenyatta amesema licha ya taifa kukumbwa na janga la Corona uchumi wa nchi umeimarika kwa asilimia 0.3 na kufikia mwezi Disemba utakuwa umepanda kwa asilimia 6.
Akigusia swala la usalama wa taifa, Rais Kenyatta amesema serikali haitakubali hata nchi yake moja kuchukuliwa na mtu binafsi ama taifa lolote lile huku akiahidi kupigania haki ya wakenya kwa kuimarishwa usalama wa taifa.
Kiongozi wa taifa ameiagiza Wizara ya elimu nchini, ile ya usalama na hazina ya kitaifa ya fedha kushirikiana na kujenga madarasa elfu 10 ili kufanikisha mpango wa asilimia 100 ya wanafunzi kujiunga na shule, akisema mtaala wa CBC utaboreshwa zaidi kwani umetengea shilingi bilioni 8.