Picha Kwa Hisani –
Rais uhuru Kenyatta ameongoza zoezi la kutoa hati miliki kwa wakaazi wa kaunti ya Nairobi.
Akizungumza katika hafla hio Kenyatta amesema serikali kwa ushirikiano na wizara ya ardhi nchini itatuatua mizozoz ya ardhi hasa katika Kaunti za Pwani kwa kutoa hati miliki kwa wamiliki wa mashamba.
Rais Kenyatta amesema kaunti za Mombasa na Kilifi zimekuwa zikishuhudia mizozo ya ardhi kutotokana ukosefu wa hati miliki kwa wamiliki halisi wa ardhi hali inayofanya wakaazi kuishi kama maskwota.
Rais amezungumza hayo jijini Nairoibi wakati alipopeana hati miliki za ardhi kwa wakaazi zaidi ya elfu 38 katika sehemu za Embakasi na Korogocho.