Picha kwa hisani –
Rais Uhuru Kenyatta amewataka wahalifu wote walio na ujuzi wa kutengeneza silaha nchini kujitokeza na kupewa ajira na serikali ya kutengeneza silaha ili kuimarisha usalama wa taifa.
Rais Kenyatta amesema hatua hiyo itasadia kiwanda cha serikali cha kutengeneza silaha katika eneo la Limuru kaunti ya Kiambu na kuhakikisha visa vya uhalifu vinasitishwa nchini.
Kiongozi wa taifa, amesema iwapo wakenya watakubali kusitisha uhalifu basi taifa hili litaimarika kiusalama na kufanikisha miradi ya maendeleo.
Rais Kenyatta ameyazungumza hayo katika chuo cha mafunzo ya polisi wa trafiki eneo la Ngong kaunti ya Kajiado baada ya kuongoza zoezi la kuteketeza bunduki haramu 5,144 zilizonashwa na polisi kutoka kwa wananchi waliyokuwa wakizimiliki kinyume cha sheria.