Story by Mwahoka Mtsumi –
Rais Uhuru Kenyatta amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufaa William Ouko kujaza nafasi ya Jaji wa Mahakama ya Upeo iliowachwa wazi na Jackton Ojwang baada ya kustaafu.
Rais Kenyatta ametoa tangazo hilo na kulichapisha katika gazeti rasmi la Serikali baada ya Jopo la makamishna 9 wa Tume ya huduma za Mahakama nchini JSC kupendekeza jina na Ouko kushikilia nafasi hiyo.
Sasa Jaji Ouko ataongeza idadi ya majaji wa Mahakama ya upeo kufikia idadi kamili ya majaji 7 baada ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu haki na sheria kumpiga msasa Jaji mkuu mteule Martha Koome.
Iwapo Jaji Koome ataidhinishwa na bunge basi Mahakama ya upeo itakuwa na idadi kamili ya majaji 7, ambapo itajumuisha Jaji Smokin Wanjala, Njoki Ndugu, Isaac Lenaola, Mohamed Ibrahim, Philomena Mwilu, William Ouko na Martha Koome.