Story by Our Correspondents –
Rais Uhuru Kenyatta amefanya kikao cha kiusalama na wakuu wa vitengo vya usalama humu nchini mda mchache tu baada ya ubalozi wa Marekeni, Ufaransa, Uholanzi na Ugerumani kutoa ilani ya tishio la kigaidi.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Msemaji wa Ikulu ya Rais Kanze Dena Mararo, wakuu hao wa usalama wamemhakikisha rais kuimarishwa kwa usalama katika kila pembe ya taifa hili.
Katika kikao hicho kilichoandaliwa katika Ikulu ya Nairobi, Rais Kenyatta amesisitiza haja ya maafisa wa usalama kujizatiti zaidi katika kuimarisha usalama wa taifa hili ikiwemo ardhini, majini na angani ili kuhakikisha taifa la Kenya iko salama.
Kikao hicho cha usalama kimehudhuriwa na Waziri wa usalama wa ndani nchini Dkt Fred Matiang’i, Inspekta mkuu wa polisi nchini Hillary Mutyambai, waratibu wakuu wa serikali, makamishna wa kaunti pamoja na wakuu wa idara zengine za kiusalama.