Picha kwa Hisani –
Rais Uhuru Kenyatta amechapisha katika gazeti rasmi la Serikali jina la Jaji Martha Koome kuwa Jaji mkuu nchini.
Rais Kenyatta amechapisha jina la Jaji Koome katika gazeti hilo mda chache tu baada ya bunge la kitaifa kuidhinisha jina la Koome katika nafasi hiyo baada ya ripoti ya bunge la kitaifa kuhusu haki na sheria kujadiliwa bungeni.
Sasa ni rasmi kwamba Jaji Martha Koome ndiye Jaji mkuu nchini na moja kwa moja anaanza majukumu yake kikatiba katika idara ya Mahakama kama Rais wa Mahakama ya Upeo na Jaji mkuu nchini.
Jaji Koome anakuwa Jaji mkuu wa kwanza Mwanamke humu nchini tangu taifa hili lijinyakulie uhuru, na kuchangia mabadiliko zaidi katika idara ya Mahakama sawia kuidhinisha mbinu mbadala za kushuhulikia kesi kwa wakati.