Story by Our Correspondents –
Rais Uhuru Kenyatta ameahidi kuimarishwa kwa usalama wa taifa hasa katika maeneo yote ya mipakani na majini ili kuhakikisha taifa linashuhudia amani na kuimarisha uchumi wa nchi.
Akizungumza wakati wa halfa ya kupandisha hadhi kambi ya jeshi ya wanamaji ya Manda Bay kaunti ya Lamu sawia na kuikabidhi bendera ya kutambulisha kikosi hicho, Rais Kenyatta amesema licha ya taifa kupokea vitisho vya kigaidi juhudi za kuimarisha usalama zitaendelezwa.
Kiongozi wa taifa amewahakikishia wanajeshi wa Kenya kwamba serikali itajitolea kikamilifu kupiga jeki usalama wa bahari kwa kuhakikisha inawapa vifaa vya kisasa vya kupambana na magaidi ili taifa liendelea kushuhudia amani, usalama na maendeleo.
Hata hivyo umeutaja ukanda wa Pwani kama utakaoboreshwa zaidi kimuundo msingi na uwekezaji kupitia miradi ya serikali ikiwemo ule wa LAPSET ili kupeyana ajira kwa vijana wengi na kuimarisha uchumi wa nchi huku akiwapongeza wanajeshi wa Kenya kwa juhudi zao za kuimarisha usalama.
Kwa upande wake mkuu wa majeshi nchini Jenerali Robert Kibochi amewapongeza wanajeshi wa Kenya kwa kujitolea kwao kulinda taifa hili huku akiahidi kupewa kipao mbele swala la usalama wa taifa.
Hata hivyo halfa hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ikiwemo Waziri wa Ulinzi nchini Balozi Monica Juma.