Picha kwa Hisani –
Rais Uhuru Kenyatta amesema sekta ya boda boda inaingiza pato kubwa zaidi kwa siku ikilinganishwa na sekta zengine nchini na kwamba iwapo itasimamiwa vyema wahudumu wa boda boda watajinasua kutoka kwa umaskini.
Akizungumza eneo la Pumwani jijini Nairobi baada ya kukutana na wakuu wa sekta ya boda boda nchini, Kenyatta amesema sekta ya boda boda upata zaidi ya shilingi milioni 980 kwa siku,bilioni 6.8 kila wiki na shilingi bilioni 357 kila mwaka.
Kenyatta amesema sekta hio ambayo inawafanyikazi zaidi ya milioni 1.4 asilimia 75 kati yao ni vijana na kwamba wakenya milioni 5.2 wanategemea sekta hio kujikimu.
Kenyatta vile vile amewataka wahudumu wa boda boda kuithamini kazi hio,kwani ni kupitia njia hio ndipo sekta hio itapata hadhi zaidi na kuongeza kipato kwa wahudumu hao.
Kiongozi wa nchi vile vile amevitaka vyama vya ushirika vya wahudumu wa boda boda kuhifadhi vyema fedha hizo ili ziwanufaishe punde wanapohitaji usaidizi wa kifedha.