Story by Our Correspondents-
Huenda uchangamoto za uhaba wa mafuta nchini zikatatuliwa baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuidhinisha kutolewa kwa shilingi bilioni 34.4 kutatua swala hilo.
Kutolewa kwa fedha hizo kumetokana na Rais Kenyatta kutia saini miswada mitano ikiwemo ule wa nyongeza ya ugavi wa fedha za ziada wa mwaka wa 2022 ambazo zitakabiliana na changomoto zinazolikumba taifa kwa sasa.
Fedha hizo zinatenga shilingi bilioni 13 ambazo zitalipwa kampuni za mafuta nchini kama ruzuku ili kufanikisha usambazaji wa mafuta sawa na kuzikabili changamoto zinazokumba kampuni hizo.
Hata hivyo katika kipindi cha juma moja wakenya wameshuhudia uhaba wa mafuta kutokana na kiwango kidogo cha mali ghafi kinachowasilishwa humu nchini kutoka kwa mataifa ya ugaibuni.
Hata hivyo siku ya Jumapili, Rais Kenyatta alisema kwamba japo swala hilo limechangiwa na vita vinavyoendelea nchini Ukraine, uhaba wa mafuta nchini utapata suluhu kwani mazungumzo ya kusitisha vita hivyo yanaendelea.