Picha kwa Hisani –
Rais Uhuru Kenyatta amelihutubia taifa na kutoa muongozo kuhusu makabiliano ya janga la Corona nchini.
Katika hotuba yake rais anatarajiwa kuondoa vikwazo vilivyowekwa kuzuia maambukizi ya corona,ikiwemo Kafyu na kufunguliwa kwa mipaka ya kenya na mataifa jirani au kuongezea muda masharti hayo.
Kenyatta atatoa hotuba hio baada ya kikao cha mawaziri na kamati maalum cha kujadili mapendekezo ya kufunguliwa shule za humu nchini ,kikao kinachoongozwa na waziri wa usalama wa ndani dkt fred matiang’i na mwenzake wa afya Mutahi Kagwe.
Wakaazi wa kaunti ya kwale tayari maoni yao kuhusu hotuba ya rais ambapo wamemtaka kiongozi wan chi kutoa muelekeo kufunguliwa kwa shule za humu nchini.
Tayari waalimu wa shule za msingi na upili kote nchini wamerejea shule hii leo kama walivyo agizwa na tume ya TSC ili kuendelea na maandalizi ya kurejelewa shughuli za masomo.