Picha kwa hisani –
Rais Uhuru Kenyatta amefanya mabadiliko katika baraza la mawaziri ikiwemo kuteua makatibu wakuu wapya wanane kuhudumu katika wizara mbali mbali.
Kwenye taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kutiwa saini na mkuu wa utumishi wa umma Joseph Kinyua,Kenyatta ameeleza kwamba mabadiliko hayo yanalenga kuboresha utendakazi ya wizara husika.
Kwenye mabadiliko hayo Kenyatta ameziunganisha wizara ya madini na wizara ya mafuta na kuwa wizara moja,huku Dkt Sara Ruto ,Eric Simiyu ,Jackson Musyoka Kalla,Lawrance Angolo Omuhaka,Japhet Micheni Ntiba,David Osiany,Zachary Ayieko na Alex Mburu wakiteuliwa kama makatibu wakuu katika wizara mbali mbali.
Katika mabadiliko hayo Dkt Belio Kipsang na mwenzake Zack Kinuthia waliohudumu kama makatibu katika wizara ya elimu wamehamishwa hadi katika wizara ya michezo na idara ya maendeleo ya kanda mtawalia,huku Gideon Mung’aro akihamishwa kutoa wizara ya ardhi hadi wizara ya ugatuzi.