Rais Uhuru Kenyatta amezindua rasmi kikosi cha ulinzi wa raslimali za baharini yaani Kenya Coast Guards.
Kwenye hotuba yake Raisi Uhuru amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kuimarisha uchumi wa taifa la Kenya.
Aidha amesema kuwa hatua hiyo itasaidia kuleta ajira kwa vijana.
Amesema kuwa kikosi hicho kitaweka ulinzi kuhakikisha hakuna uingizaji wa madawa ya kulevya sawia na kukabiliana na wavuvi haramu.
Akigusia swala la uvuvi Uhuru amezitaka ardhi ambazo zinashikiliwa na wavuvi wa kibinafsi kurudisha kwa serikali ifikapo mwezi Machi mwaka ujao.
Naye Naibu rais William Ruto amesema kuwa uzinduzi wa kikosi hicho kitaimarisja uhifadhi wa chakula wa taifa hili.
Kwa upande wake waziri wa usalama wa ndani Fred Matiangi amasema kama idara ya usalama iko tayari kukabiliana na wavuvi haramu nchini sawia na kulinda raslimali za baharini ili kuona kwamba hazitumuki vibaya basi zinasaidia kuimarisha uchumi wa taifa.
Taarifa na Hussein Mdune.