Picha kwa hisani –
Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga hii leo ameanza ziara yake ya siku mbili katika Kaunti ya Taita taveta.
Raila atapokelewa na mwenyeji wake ambaye ni Gavana wa Taita Taveta Granton Samboja huko Wundanyi na kisha kuendelea na ziara yake katika maeneo ya Taveta na Voi.
Kiongozi huyo ambaye amekuwa mwandani mkuu wa Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kukutana na Viongozi wa chama cha ODM eneo hilo sawa na kuupigia debe mchakato wa BBI.
Ziara ya Odinga katika Kaunti ya Taita taveta inaanza wakati Serikali inakabiliwa na mabishano makali ya kisiasa huku Chama cha Jubilee kikionekana kugawanyika.