Picha kwa hisani –
Naibu wa rais William Ruto amezidi kumkashifu kinara wa ODM Raila Odinga kwa madai kwamba ushirikiano wake na Rais Uhuru Kenyatta umechangia pakubwa kusambaratika kwa chama cha Jubilee.
Akizungumza baada ya kuongoza shughuli ya kufungua kituo kipya cha polisi katika eneo la Mwangulu huko Lunga lunga Ruto amesema baada ya ushirikiano huo jubilee imeshindwa kufanikisha ajenda zake za maendeleo.
Kwa upande wake mwakilishi wa kike kaunti ya taita taveta Lydia Haika na mwenzake mbunge wa Nyali Mohamed Ali ,wameutaja mchakato wa BBI kama usio na manufaa wakiwataka wananchi kuupinga.