Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga ameshikilia kwamba mradi wa Galana Kulalu utasaidia pakubwa taifa kuwa na usalama wa chakula iwapo utasimamiwa vyema.
Akiongea baada ya kukagua mradi huo Odinga amesema wanakandarasi wanaoendeleza mradi huo wamewajibika katika kuufanikisha licha ya kukumbwa na changamoto.
Kwa upande wake Gavana wa kilifi Amason Jefa Kingi aliyekua ameandamana na Odinga ameeleza masikitiko yake kwamba malengo ya kuanzishwa kwa mradi huo yamekosa kufanikishwa.
Hata hivyo mwenyekiti wa bodi ya unyunyizi nchini Ngugi Toro amesema wako tayari kusimamia mradi huo kuhakikisha unaafikia malengo ya kuwepo kwa usalama wa chakula na kumaliza baa la njaa nchini.