Picha kwa Hisani –
Raia watatu wa taifa la Ethiopia pamoja na mkenya mmoja wametiwa nguvuni na maafisa polisi kwa kuingia humu nchini kinyume cha sheria.
Akithipitisha kutiwa nguvuni kwa watu hao, Kamanda wa Polisi kaunti ya Kwale Joseph Nthenge amesema watu hao wamepatikana katika nyumba ya Mwahiu Nyamawi katika kijiji cha Kiwegu eneo la Vanga kaunti ya Kwale.
Nthenge amewaonya wakaazi dhidi ya kuendeleza biashara ya ulanguzi wa binadamu, akisema watakaopatikana watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Hata hivyo watu hao wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani hapo kesho.