Picha kwa hisani –
Idara ya usalama katika kaunti ya Kwale imewataka raia wa Tanzania wanaoishi karibu na mpaka wa kenya na Tanzania eneo la Lunga lunga kutoingia humu nchini kwa njia zisizo halali.
Kamishana kaunti ya Kwale Joseph Kanyiri amesema baadhi ya raia wa mataifa ya kigeni wanatumia njia za mkato kupenya humu nchini,akisema raia wa kigeni wanapaswa kupitia mipakani ili kukaguliwa kabla kuruhusiswa kuingia nchini.
Kanyiri amesema wameeka maafisa wa kutosha katika mpaka wa kenya eneo la lunga lunga ili kuhakikisha raia wa kigeni hasa kutoka taifa jirani la Tanzania wanapimwa virusi vya Corona kabla kuingia nchini.
Kanyiri amesema wizara ya afya nchini itaidhinisha mipangilio kati ya yake na taifa jirani la Tanzania ya jinsi ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona kati ya mataifa hayo mawili.