Wanamuziki kumi na mmoja kutoka Pwani ya Kenya wameshirikiana na kuachilia ngoma yao mpya inayoitwa Corona. Wimbo huu unaelezea hali ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini pamoja na kuielimisha jamii kuhusu jinsi watakavyoweza kupunguza usambazaji wa ugonjwa huu ambao ni janga la kimataifa.
Wasanii hao kumi na moja ni pamoja na Sanova kutoka Kwale, Davy Gze kutoka Likoni, Fat-S kutoka Likoni, Dogo Richie kutoka Bamburi, Ziky Mtanah kutoka Kinango, Denno Mkali kutoka Mariakani, Happy C kutoka Kaloleni, Mnyamwezi kutoka Malindi, Medallion kutoka Kilifi, Mlole Classic kutoka Taveta na Ally B kutoka Mishomoroni.
Wimbo huo wa dakika tano umetengezwa na Producer Bang Belly kutoka recording label ya Waghetto. Kupitia kwa njia ya simu na Radio Kaya, Bang Belly amewashukuru pia producer wengine wakiwemo, Dhilly Dhilly kutoka Cracksound records, Emmy D kutoka Dallaz records, Burning Ice kutoka Trace Music, Sherrif na Mobiz kutoka Tundersound records, MPK kutoka upward music na Sanova kutoka Nova records, ambao walihusika kuwarecord wasanii kutoka maeneo ya mbali na kumtumia vocals zao ili aziunganishe kwa wimbo mmoja.
Kupitia kwa njia ya simu na Radio Kaya, Producer Bang Belly alifichua kwamba walishirikiana na watangazaji wa kipindi cha Kaya Flavaz, Robby Dallaz na Caroline Mkamburi kuandaa ngoma hiyo. Pia, aliishukuru stesheni hiyo kwa kuufadhili mradi huo na kwa kuwa mstari wa mbele kukuza vipaji vya wasanii wa Pwani.
This is awesome, keep up with the spirit radio kaya.