Kituo cha Raido Kaya kimeshinda tuzo la kituo bora zaidi kwa kuangazia maswala ya athari za mihadharaiti kwenye mashindano ya Wanahabari yalioandaliwa na Shirika la kupambana na utumizi wa Mihadarati la Reach out Centre Trust.
Kwenye mashindano hayo yaliyoandaliwa mjini Mombasa, kati ya vituo 10 vya uwanahabari, Radio Kaya iliweza kubeba tuzo hilo kwa kuhusika pakubwa kwenye maswala ya kuielimisha jamii kuhusiana na athari ya dawa ya kulevya.
Katika upande wa Uwanahabari bora kwenye tuzo hizo, Gabriel Mwambeyu kutoka Radio Kaya alishinda tuzo la Mwanahabari bora aliyejitolea kupiga vita Mihadarati huku Dominick Mwambui akishinda tuzo la kitengo cha watangazaji bora kwenye maswala ya dawa ya kulevya.
Akiongea kwenye hafla ya kuwazawadi Wanahabari, Mkurukenzi mkuu wa Shirika la Reachout Center Trust, Taib Abdulrahman amekitaja kituo cha Radio Kaya kama chenye manufaa kwa jamii kupitia juhudi zake za kuielimisha jamii kuhusu athari za mihadarati.
Kwa upande wake Meneja wa kituo cha Radio Kaya Victor Ongwena amesema atahakikisha juhudi zaidi zinaekezwa katika kuielimisha jamii kuhusu jinsi ya kujiepusha na utumizi wa mihadarati kwa ushirikiano na Shirika la Reachout Center Trust.
Hata hivyo kwenye sherehe hizo zaidi ya wanahabari 50 waliweza kushiriki kwenye mashindano hayo.
Taarifa Hussein Mdune.