Katika juhudi zake za kujiweka vyema kwa ajili ya mawimbi makali ya ushindani wa utangazaji ukanda wa Pwani Radio Kaya imeimarisha kikosi chake cha utangazaji.
Kikosi hicho sasa kitajumuisha mtangazaji Dominick Mwambui na Hamisi Managale.
Mwambui amekuwa akiendesha kitengo cha michezo katika kituo hicho kwa muda wa miaka miwili na nusu baada ya kuchukua mikoba kutoka kwa Salim Mwakazi.
“Kila hatua hutathminiwa na uamuzi kufanywa kwa sasa imebidi tuimarishe kitengo kwani majukumu yamekuwa mengi kwangu,” amesema Mwambui.
Kwa sasa Hamisi atakuwa akisukuma gurudumu la Matukio Viwanjani akisaidiana na Mwambui ambaye amepewa jukumu jipya katika kituo hicho.
Taarifa na Michael Otieno.